Kwa mujibu wa mwandishi wa ABNA akitoa taarifa kutoka China Daily, wakati mvutano katika eneo hilo ukiendelea, meli kadhaa zimevuka Mlango wa Hormuz kwa kutekeleza itifaki za usimamizi zilizowekwa na Iran.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli kadhaa ikiwemo meli za China kwa uratibu uliofanywa na ndani ya mfumo wa kanuni za usimamizi wa trafiki katika njia hiyo ya kimkakati ya maji zimevuka Mlango wa Hormuz; hatua inayoonyesha jukumu muhimu la Iran katika usimamizi wa trafiki ya baharini katika njia hiyo muhimu.
Walinda Mapinduzi wa Kislamu wa Iran pia katika taarifa yao walitangaza: Baada ya ombi la upande wa China na makubaliano juu ya itifaki za usimamizi wa mlango huo, meli kadhaa za nchi hiyo zilipata ruhusa ya kuvuka njia hiyo, na mchakato wa kuvuka kwao umeanza tangu usiku wa jana.
Licha ya hayo, kiwango cha trafiki cha meli bado kinakadiriwa kuwa chini kuliko kiwango cha kawaida kabla ya mvutano. Hapo awali, kwa wastani takriban meli 140 kwa siku zilivuka Mlango wa Hormuz, lakini sasa idadi hiyo imepungua. Wakati huo huo, Iran imetangaza kuwa hadi sasa zaidi ya meli 30 zimepewa mwanga wa kijani (ruhsa) kuvuka mlango huu.
Ripoti zinaonyesha kuwa meli kadhaa zimesafiri kwenye Mlango wa Hormuz kwa kutekeleza itifaki za usimamizi za Iran, ingawa kiwango cha trafiki cha baharini bado ni cha chini kuliko hapo awali.
Your Comment